Hizi ni simulizi za kusisimua, kuelimisha na kuburudisha zikiakisi maisha kwa ujumla.
Soma kupitia tovuti yetu
Pakua app yetu kutoka playstore
Pakua app yetu ya android
Marco Tibasima ni mchoraji, mbunifu na mwandishi wa hadithi aliyeshinda tuzo mbalimbali kutoka Tanzania. Yeye ni manii mwenye kipaji. Kazi yake inavutia watazamaji wa kila rika na kizazi. Amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 25 kama msanii wa kujitegemea kwa NGOs, watu binafsi, Mashirika ya Serikali na makampuni ya biashara. Amechora majarida mbalimbali kama vile SANI, AMBHA, TABASAMU nk.
Tibasima Comics inajumuisha watunzi na wachoraji mbalimbali wabobevu wa kitanzania. Baadhi ya watunzi hao ni Ally Mbetu, Oscar Ndauka, Mohamed Lupinga, Fortunatus Ndilla, Dick Mau Mponda na wengine wengi. Baadhi ya wachoraji hao ni Marco Tibasima, Aloys Mabina, Aloyce Jacob, Shauri Kati, Theophil Mnyavanu, John Nganyanyuka na Jimmy Washa. Kazi zao zimekuwa maarufu sana kwenye magazeti, majarida na vitabu mbalimbali nchini Tanzania.
Hizi ni simulizi za kusisimua, kuelimisha na kuburudisha zikiakisi maisha kwa ujumla.
Huu ni mfululizo wa simulizi za Mti Mkavu. Mganga wa kienyeji mwingi wa hila kwa wateja wake, hasa wanawake. Ungana nasi kuusoma kuanzia toleo hili hadi mwisho wa mkasa huu. Ni Hila za MTI MKAVU!
Jarida lenye mkusanyiko wa katuni na simulizi kwa kutumia michoro. Linatoka kila siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.